RWANDA AFTER GENOCIDE IPO MADUKANI


Ile Filamu Mliyokua Mkiisubiri Kwa Hamu  ambayo ilizuiliwa na bodi ya filamu,Movie Hiyo Inaitwa RWANDA AFTER  GENOCIDE (Rwanda Baada Ya Vita) Sasa Ipo Madukani Huku Ikiwa Imeandaliwa Na Mmiliki Wa Kampuni Ya Freedom Distributors Ignatios Kambarage ambaye Pia Ndiye Aliyetunga story nzima pamoja na kuandika script na kudirektiwa  na yeye mwenyewe
PATA NAKALA YAKO SASA

JELA IMEMBADILISHA LULU,HII NDO KAULI YAKE JUU YA BABU SEYA NA MWANAE



“Ninaamini Mungu yupo...anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki...!!!!Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha...!hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu...Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo...!Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu...!AMEN”
Hayo ni maneno ya mwanadada Elizabeth Michael (LULU) aliyoyaandika kupitia kwenye mtandao akiwaombea kheri Mzee Nguza na mwanawe Papii Kocha wanaosubiria kusikilizwa kwa rufaa yao ya kesi ya ulawiti inayowakabili
Toka atoke jela, mwanadada lulu ameonekana kubadilika sana kitabia tofauti na alivyokuwa akionekana hapo awali.

JE WANAJESHI WA KENYA WALIIPORA WESTGATE?



Mmoja wa wanamgambo wa Al Shabaab wanaosemekana kuuawa kwa shambulizi la Westgate
Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.
Hata hivyo haijulikani walichokuwa wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka yao bbaada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wangambao wa Al Shabaab waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.

CHANZO:BBC

MOVIE NAME:SWEET & BITTER | UNDER FREEDOM DISTRIBUTORS


Tash Anasalitiwa Na Kila Mwanamke Mwishowe Anaamua Kutopenda Tena Na Kuanza Kutembea Na Machangudoa Hatimaye Anapata Ugonjwa Wa Ukimwi Hivyo Anaona Bora Alipize Kisasi
JE ATAFANIKIWA?FATILIA MKASA HUU

KAMBARAGE:SASA AFYA YANGU INAELEKEA KUIMARIKA,NI BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA YA PIKIPIKI


Msemaji wa Kampuni ya Steps na mmiliki wa blog na kamPuni  ya Freedom Distributors Bwana Kambarage Ignatios Alipata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya Tazara Siku Ya Jumapili Ya Tarehe 27 na kukimbizwa katika hospitali ya Taifa Ya Muhimbili na Kupatiwa Matibabu Ya Haraka Ambayo Yamefanikisha Hadi Sasa Afya Yake Kuimarika na Kupelekea Kupewa Ruhusa Ya Kurejea Nyumbani .Majeraha Aliyoyapata ni katika maeneo Ya Kichwani Mguuni Zifuatazo Na Picha Muda aliokuwa amelazwa Hospitali
Jeraha Alilopata Maeneo Ya Mdomoni